Morrison ataja figisu zilizomwondoa Simba, aitaja Yanga

0
12

Benard Morrison amesema anadhani moja ya chanzo cha yeye kuwa nje ya Simba SC ni baada ya kutosaini mkataba aliopewa na uongozi wa timu hiyo kabla ya michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu.

Amesema Desemba 2021 hadi Januari mwaka huu alikwenda nchini Ghana kushughulikia masuala ya familia, na aliporudi Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdalah
(Try again) alitaka ampe mkataba mpya lakini Morrison alimwambia wamalize kwanza michuano ya kombe la Mapinduzi kisha watazungumza, lakini haikuwezekana tena.

Aidha, amesema chanzo kingine ni baada ya yeye kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Yanga SC, lakini uongozi haukumpa uangalizi mzuri na kumlazimu ajiangalie mwenyewe, hali iliyopelekea kutohudhuria mazoezi kwa siku kadhaa.

Amedai baada ya kutohudhuria mazoezi, kocha wa timu hiyo alimkasirikia takribani siku saba kwa sababu hakutoa taarifa na ndipo Mkurugenzi Mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez alipomuita ofisini na kumwambia kuwa wachezaji na kocha wanachukizwa kwa sababu ya utovu wake wa nidhamu.

“Alisema wachezaji wanalalamika kwamba hawataki nihudhurie mazoezi na makocha wanalalamika kuwa siwaheshimu, hivyo malalamiko yamezidi, nikasema hapana sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo, kwa sababu nilipokuwa siji mazoezi walikuwa wananipigia wakiniuliza naendeleaje na majeraha yanaendeleaje, kama kuna kitu chochote unataka uniambie niambie moja kwa moja,” amesema.

Hata hivyo amebainisha sababu za kurudi Tanzania kuwa ameona ni vyema zaidi kama atakutana na uongozi wa Simba na bodi ili kuwaaga badala ya kuwasiliana nao kwenye simu.

Morrison ameongeza kuwa anaipenda klabu ya Simba na anapenda kufanya nao kazi lakini kwa sasa kuongezewa mkataba mpya ni vigumu.

Send this to a friend