Moto wazuka Mlima Kilimanjaro

0
58

Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana umezuka katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuzua taharuki kwa wakazi wa mji wa Moshi.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi usiku wa Oktoba 21, 2022 Ofisa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA), Charles Ng’endo amethibitisha kutokea kwa moto huo akisema unaonekana kuanza majira ya jioni.

Aidha, ameeleza kuwa eneo ambalo moto huo unaonekana ni eneo la Millenium na katika bonde la Karanga ambapo amesema wanapanda kupitia geti la Mweka ili kuuzima.

Send this to a friend