Mpangaji adaiwa kumuua mwenye nyumba kwa madai ya kodi

0
48

Mkazi wa Kijjiji na Kata ya Likongowele, wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Siamini Mtopoka (40) amedaiwa kuuawa na mpangaji wake aitwaye Shabani Matola kwa  kukatwa na panga Februari 05, 2023  kwa madai ya ugomvi wa malipo ya kodi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha tukio hilo ni baba mwenye nyumba kufika alikokuwa anaishi mpangaji huyo kumdai malipo ya pango la nyumba ambapo madai hayo yalikataliwa na mtuhumiwa baada ya kumweleza kuwa endapo anataka kodi yake basi amlipe kwanza fedha alizokuwa anamdai kutokana na kazi aliyokuwa amempa ya kubangua korosho.

Muumini alitaka kanisani kumrudishia zaka zake akidai hana mpango tena wa kwenda Mbinguni

Wamedai kauli ya mpangaji huyo haikumfurahisha mwenye nyumba na ndipo alimfungia mlango kwa ndani na kuamua kwenda kumshitaki kwenye ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata, kisha mtuhumiwa huyo aliamua kuvunja mlango na kumfuata mwenye nyumba akiwa na panga mkononi na ndipo alipompiga panga kichwani na kufariki.

Aidha, Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Pili Mande amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba mtuhumiwa huyo yuko chini ya polisi ambapo upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend