Mpiga kinubi aweka rekodi ya dunia Mlima Kilimanjaro

0
77

Mpiga kinubi maarufu kutoka nchini Ireland, Siobhan Brady ameweka rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kupiga kinubi kwa dakika 34 akiwa kileleni futi 19,000 juu ya Mlima Kilimanjaro.

Mwanamuziki huyo maarufu awali alipiga kinubi akiwa futi 16,000 katika Mlima Himalaya nchini India mwaka 2018, ambapo aliweka rekodi kwa kupiga kinubi kwa dakika 18.

Bondia Mayweather atumika katika kampeni za uchaguzi Zimbabwe

Kamati ya Guiness inasubiriwa kuthibitisha rekodi hiyo inayotambulika kama ‘Guiness World Record for the Highest Harpist Concert.’

Brady akiwa na timu yake alianza safari ya kupanda kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 20, mwaka huu kupitia geti la Machame.

Send this to a friend