Mpina ataka uchaguzi usifanyike hadi mahakama itakapotoa uamuzi wa rufaa yake

0
92

Mwanachama wa Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina ameitaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kusitisha uchaguzi wa nafasi ya Rais mpaka pale Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi juu ya rufaa yake ya kupinga kuondolewa kugombea Urais.

Mpina alikata rufaa kupinga kuondolewa kwenye orodha ya wagombea Urais wa Tanzania baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu Dodoma kutupilia mbali kesi ya kikatiba aliyoifungua pamoja na ACT – Wazalendo, kwa kile mahakama ilichoeleza kuwa haina mamlaka ya kuingilia uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

“Nasisitiza kuwa ni muhimu sana uchaguzi wa nafasi ya Rais usifanyike hadi hapo Mahakama ya Rufaa itakapokuwa imetoa uamuzi juu ya rufaa yangu,” amesema.

Aidha, Mpina amesema kinachompeleka mahakamani si kurudishwa kwenye orodha ya wapiga kura kwenye nafasi ya urais, isipokuwa anapigania muktadha wa vyama vya upinzani na kupata heshima inayostahili kwenye taifa.

Send this to a friend