Mraba wa wikiendi: Dalili 10 kwamba umekutana na mwanamke wa maisha yako

0
49

Wikiendi hii mraba huu unagusa hasa wanaume. Sote tunajua namna gani wanaume wanavyoota na kujitahidi kwa kila mbinu kumpata msichana wa kuingia naye kwenye mahusiano ambaye anakidhi vigezo unavyokuwa umejiwekea. Haijalishi ni mara ngapi unaingia kwenye mahusiano, kila mara lazima utakuwa unatafuta mtu ambaye ni “perfect” flani hivi kwa standards zako. Wakati mwingine unaingia kwenye mahusiano kama kuskilizia hivi kuona kama huyu ndiye wa maisha au siye. Sasa leo mimi nakuchambulia mambo 10 ya kuangalia ili kujua kama uliye naye ndiye dream woman wako au hapana. 

  1. Anakupa uhuru binafsi?

Kuna mwanamke ukiwa naye kwenye mahusiano kila dakika anakuwa kama kakukalia shingoni. Muda wote anacheki status gani umeweka, anataka passwords zako, anataka ajue kina nani leo umeongea nao na mambo mengine mengi ambayo hadi yanachosha. Mwanamke lazima akuamini na kukupa nafasi (personal space) kuishi maisha yako pia huku mahusiano yakiendelea. Personal space ni njia moja kuonyesha kwamba anakuamini na anaamini maamuzi na mwenendo wako. Kama hilo halipo basi hapo ulipo pana shida. 

2. Anajiamini?

Asiwe feki. Ajiamini kwa kile alicho nacho iwe sura, umbile, elimu au kipato. Kimbia mbio za hela yote ukikutana na msichana ambaye ana-fake maisha. Hiyo ni dalili kwamba mkiamua kuishi pamoja kuna mengi mtafeli huko mbele. Atataka afeki ninyi ni wa nyama choma na bia wakati uwezo wenu ni Fanta na Chipsi Kavu. Mwisho mtashindwa kufanya mengi ya msingi kwenye maisha sababu mnaishi kipato kisicho chenu (beyond your means). 

3. Anaheshimu familia yako na marafiki zako?

Hii na wewe unapaswa kufanya vivyo hivyo. Dream girl lazima aheshimu familia yako na marafiki zako wa karibu. Kumbuka kuwa ninyi siku moja mtakuwa familia na Kiafrika tunaishi tukiendeleza mahusiano na familia zilizotukuza mpaka tukawa watu. Mwanamke asiyeheshimu familia yako na ulipotoka anakutenga na dunia yako na kukufanya uwe mkosefu wa shukrani. Lazima kujenga mahusiano bora za familia za pande zote mbili na ukiwa na msichana ambaye haelewi hilo basi umeingia kwenye matatizo.

4. Unajisikia maisha yako yamebadilika baada ya kukutana naye?

Angalia unamuwaza mara ngapi? Mara ngapi ukiwaza mipango ya maisha na yeye unamuona ndani ya hiyo mipango? Mwanamke wa maisha yako huwa anakuingia kichwani na unaanza kumuona ndani ya maisha yako. Ukiona uko na mwanamke na humuoni ndani ya fikra zako za mipango ya baadaye au huhisi maisha yako yamebadilika hata kimawazo basi jichunguze vizuri.  

5. Akisikia mtu anakusemea mbovu mahali anakwambia?

Kakangu, mwanamke ambaye anakutaka hasa uwe ndani ya maisha yake hawezi kuficha jambo analolisikia mahali kuhusu wewe. Kuna cases unakuta unasemwa mahali vibaya halafu mwanamke wako haji kukwambia, hiyo dalili mbaya. Mwanamke wa maisha yako ukisemwa wewe na yeye anaona kasemwa maana anaamini ninyi ni wamoja. 

6. Hakuna siri

Hii inaendana kiasi na namba 5 hapo juu. Msichana wa maisha yako hakufichi siri. Atakuficha siri kama kuna sehemu anajua kila mtu atachukua njia yake. Kama ninyi ni wamoja na mtadumu maisha kuna sababu gani ya kuficha siri? Weka mambo wazi tuyaishi pamoja. Ukweli unakuweka huru. Akianza kukuficha mambo sasa hivi huku mbele unajua atakuficha nini kingine?

7. Anajua nafasi yako?

Mwanaume ni kichwa cha mahusiano na familia. Anafahamu hivyo? Anaheshimu? Na wewe jua kwamba ni kichwa na behave kama kichwa. Sio unakuwa na mambo ya kijinga jinga halafu unadhani utapewa heshima ya ukichwa. Kama kila jambo unafanya sahihi katika nafasi yako hiyo, anakupa heshima unayostahili? Anasikiliza maoni yako? Anakushirikisha kupata mawazo yako kabla ya kuamua mambo? Mahusiano yanayodumu hutokana na kuheshimiana na kila mmoja kutambua nafasi yake na ya mwenzake na kuziishi.

8. Anabadilika kuendana na hali yako?

Siku ya ugali dagaa anakula bila kununa? Namaanisha siku mambo yakiwa hivyo mfukoni anaelewa na mnaishi kuendana na hali iliyopo? Ukiona haelewi na muda wote anataka muwe juu tu fahamu kuna tatizo. Maisha ni milima, mwanamke wa ndoto zako atakuwa na wewe kwa roho safi na kukutia nguvu katika hali zote. 

9. Unamuona ni kimbilio lako la kukupa amani?

Hii ni mfano inatokea kazi, biashara, etc vimekuvuruga siku hiyo na unahisi kichwa kinataka kupasuka. Ukienda kukutana naye unapata amani na kutulia kiasi fulani? Ukiona ni mwanamke wa namna hiyo basi ndipo penyewe. Mwanamke wa ndoto zako huwa ni tulizo kipindi cha mawimbi na dhoruba za maisha. 

10. Anaamini?

Kwamba wewe na yeye kama timu mnaweza kufikia malengo kwenye maisha kama mkiwa pamoja, kujaliana na kushirikiana? Kama hana hiyo imani na anasitasita kuna tatizo. Mwanamke wa maisha yako yuko optimistic, anaamini no matter mko level gani, kama mkishikana kama timu pamoja mtafika mbali. Atakutia moyo kwenye mihangaiko yako, atajitahidi asiwe mtapanyaji wa unachopata na atakuombea mafanikio kwa Mungu. 

***End**

Nancy Kifani

Saint Augustine University, Mwanza

Send this to a friend