Mradi wa umeme wa Kigagati-Murongo kufungua zaidi uchumi wa Kagera

0
31

Rais Samia Suluhu Hassan amesema umeme unaozalishwa katika mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, unaotekelezwa katika bonde la Mto Kagera utaboresha shughuli mbalimbali za kibiashara pamoja na kuongeza uwekezaji zaidi nchini.

Akizungumza leo katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo nchini Uganda akiambatana na mwenyeji wake Rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni amesema nishati hiyo itakwenda kuweka usawa kati ya jamii za mijini na vijijini.

“Nishati ya umeme inakwenda kuongeza ulinzi katika maeneo yetu kwa ujumla, nishati pia itakwenda kupunguza pengo la kukosekana kwa usawa kati ya mijini na vijijini, wote watafurahia manufaa sawa,” amesema.

Waziri asema hali ya usalama mpaka wa Tanzania na Msumbiji haitabiriki

Ameongeza kuwa “nishati inayozalishwa hapa itaboresha biashara na uwekezaji katika ukanda huu, itaboresha usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa pamoja na shughuli zote za biashara.”

Aidha, amesema kwa sasa Tanzania imejikita katika usambazaji wa umeme vijijini, hivyo nishati zinazozalishwa zitakwenda kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha vijiji vinafikiwa na nishati hio ya umeme.

Naye Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewataka wananchi kuacha kubishana juu ya nani anachukua nishati nyingi kati ya Tanzania na Uganda, na kueleza kuwa ikiwa Tanzania itaomba kupewa nishati nyingi zaidi haitokuwa tatizo kwakuwa nishati hiyo inalipiwa.

Send this to a friend