
Tetesi kuhusu mrithi wa Papa Francis zimeanza baada ya kifo chake, huku Kardinali Robert Sarah kutoka Guinea akitajwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa.
Kuna uwezekano kuwa Papa ajaye atatoka katika maeneo kama Afrika, Italia, Sri Lanka au hata Amerika. Iwapo atachaguliwa Kardinali Robert anayetimiza miaka 80 mwezi Juni, atakuwa Papa wa kwanza Mwafrika tangu karne ya tano.
Kardinali Robert, amekuwa akikosoa baadhi ya maamuzi ya Papa Francis akiungwa mkono na makundi ya kihafidhina ndani ya Kanisa Katoliki.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa sheria za kanisa, Edward Peters, anasema kikanuni, mwanaume yeyote aliyebatizwa anaweza kuchaguliwa kuwa Papa, na iwapo mtu huyo hajapewa daraja la ukuhani, ni lazima awekewe mikono na kupewa cheo cha askofu ili uchaguzi wake uwe halali.