Msaidizi wa Bernard Membe ahojiwa kwa utakatishaji fedha

0
51

Jerome Luanda ambaye ni msaidizi wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Bernard Membe, anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kwa tuhuma za utakatishaji fedha.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hilo leo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu alipo Luanda ambaye ilielezwa kuwa alitekwa.

“Na huyu nasema amekamatwa na anahojiwa kwa kosa la kutakatisha fedha,” amesema Mambosasa.

Ameongeza kuwa madai kuwa Luanda alitekwa na watu wasiojulikana hayana ukweli wowote.

Send this to a friend