Msajili: Ni mkutano wa wadau, sio wa Rais na vyama vya siasa

0
54

Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa mkutano wa siku tatu utakaofunguliwa leo kujadili hali ya demokrasia na siasa nchi, sio mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na vyama vya siasa, bali ni mkutano wa wadau wasiasa.

“Wengi wanakosea wakifikiri ni mkutano wa Mhe. Rais ana vyama vya siasa, hapana,” amesema Jaji Mutungi na kusema mkutano huo ni wa wadau lakini utafunguliwa na Rais Samia na kufungwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Aidha, amesema siku ya Rais kuzungumza na vyama vya siasa itapangwa ili wapate nafsi ya kueleza masuala yatayowezesha kuimarisha demokrasia nchini.

Ameongeza kwamba mkutano huo utakaoanza leo Desemba 15 hadi 17 mkoani Dodoma utahusisha watu na taasisi zote ambazo shughuli zao zinahusisha siasa, lengo likiwa kujadili hali ya demokrasia ya vyama vingi nchini.

Licha ya wito wake wa kutaka wadau wote kushiriki, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi vimekataa kushiriki vikao hivyo kwa maelezo kwamba baadhi ya matakwa yao hayajatimizwa.

Send this to a friend