Msajili: Vyama vya siasa haviruhusiwi kuungana ghafla wakati wa uchaguzi

0
51

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza, amesema kuwa vyama vya siasa haviruhusiwi kuungana ghafla wakati wa uchaguzi kwani sheria ya vyama vya siasa inawekwa kwa maslahi ya wanachama na wananchi hivyo haviruhusiwi kufanya kitu cha kuhadaa watu.

Akizungumza katika kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio amevitaka viasa vyama vya siasa vinavyotaka kuungana siku ya Oktoba 3 mwaka huu, kuacha mara moja mpango huo kwani wanakiuka utaratibu wa sheria na kwamba walianza vizuri hivyo ni vyema kila mmoja akaendelea kunadi sera zake.

Sisty ameongeza kuwa tayari Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekwishaviandikia barua vyama hivyo.

“Ukiunganisha nguvu na chama kingine wakati mmeshakubaliana na wananchi kwamba mtatekeleza sera gani ni kuwahadaa, sisi tulishawasiliana nao na tukawaambia waache.”

Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na tetesi kuwa vyama vya ACT-Wazalendo na CHADEMA vikitaka kushirikiana kwa kuwa na mgombea mmoja wa Urais.

Send this to a friend