Msajili wa Hazina na CAG kushirikiana katika usimamizi wa mashirika ya umma

0
2

Ikiwa ni sehemu ya dhamira na jitihada za kuhakikisha taasisi na mashirika ya umma yanaongeza mchango katika ustawi wa uchumi wa Taifa, Ofisi ya Msajili wa Hazina na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi zimekubaliana kushirikiana katika maeneo nane ya kiusimamizi.

Maeneo waliyokubaliana kushirikiana ni utawala bora, ufanikishaji wa utekelezwaji wa mapendekezo ya ukaguzi, kuboresha mifumo ya usimamizi na uongozi, usimamizi mzuri wa rasilimali za umma, uwajibikaji wa kifedha, kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R4 za Rais Samia Suluhu.

Makubaliano hayo yalifikiwa katika kikao kazi cha siku mbili kilichoanza  Jumanne, Februari 25, 2025 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, iliyopo Kibaha, Mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, hadi kufikia Juni 30, 2024, Serikali ilikuwa imewekeza kiasi cha TZS trilioni 86.3 katika taasisi 308 ambazo inazisimamia, ikiwemo zile ambazo ina hisa chache. Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na Sh75.6 trilioni, kiasi kilichowekezwa hadi kufikia mwaka 2023.

“Tulijadili kuhusu kuboresha uwajibikaji wa kifedha na utekelezaji  wa maazimio mbalimbali yanayolenga kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora,” amesema CAG, Charles Kichere .

Pia katika Mkutano wa Ofisi hizo mbili wmekubaliana kushirikiana linapokuja suala la kuhakikisha taasisi za umma zinatekeleza mapendekezo ya ukaguzi  ‘Audit recommendations’.

Send this to a friend