Msajili wa vyama vya siasa akanusha kuzuia mikutano ya ndani

0
74

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania, Jaji Francis Mutungi amesema kanusha taarifa zilizotolewa kwamba ametoa amri ya kusitishwa kwa mikutano ya ndani ya vyama vya siasa.

Katika ufafanuzi wake alioutoa leo Jaji Mutungu amesema “hilo halina ukweli wowote na niwasihi mlipuuze kwa uzito unaostahili.”

Amesema hajatoa amri hiyo na kwamba waliopotosha taarifa yake wamefanya hivyo kwa sababu wanazozijua wao au kwa kutokuelewa vizuri alichokisima.

Amefafanua kuwa katika taarifa yake amevishauri vyama vya siasa katika kipindii ambacho wanajaribu kupata suluhisho la mivutano, vyama hivyo vijizuie kwa muda kuendelea na shughuli zilizosababisha kutoka kwa mivutano hiyo.

Wakati ofisi yake ikiendela na jitihada za kuitisha mkutano huo kati ya ofisi yake, vyama vya siasa na jeshi la polisi, tayari CHADEMA imeweka wazi kwamba haitoshiriki kikao hicho.

Send this to a friend