Msako wa mifuko ya plastiki kuanza Jumatatu

0
50

• Operesheni ya kukamata mifuko ya plastiki iliyozuiliwa kuanza rasmi Jumatatu jijini Dar es Salaam .
• Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameelekeza msako wa mifuko ya plastiki ufanyike Mikoa yote.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla ameelekeza operesheni ya kukamata mifuko ya plastiki iliyokatazwa kuanza rasmi Jumatatu Agosti 29, 2022 kwenye masoko yote ya Mkoa huo.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao na viongozi wa masoko yote ya Dar es Salaam, machinga na maafisa masoko ambapo ameelekeza msako wa kukamata wiwanda vinavyozalisha mifuko hiyo kuanza mara moja.

Karani ajiua saa chacha kabla ya sensa, aacha ujumbe

Aidha, ameelekeza kila Wilaya kupitia kamati za ulinzi na usalama kuendesha operesheni hiyo, na kuwataka maafisa masoko kwa kila soko kutoa taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo kwa Mkurugenzi wa halmashauri husika kila siku.

Pamoja na hayo, RC Makalla ameelekeza mamlaka za udhibiti ikiwemo Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na TBS kutoa tamko la maelekezo ya usimamizi kwa kila Mkoa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha elimu inaendelea kutolewa.

Ameongeza kuwa, tayari amepata baraka zote za operesheni hiyo kutoka kwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ambae ameelekeza kila Mkoa kufanya operesheni ya kutokomeza na kuzuia uingiaji wa mifuko hiyo.