Msanii aitaka kampuni ya mabasi imlipe milioni 123 na kwa kutumia wimbo wake

0
26

Msanii wa Kizazi kipya, Nuni Suleimani (35) ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Arusha kuiamuru kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Track kumlipa fidia ya shilingi milioni 123 baada ya kutumia wimbo wake kwenye matangazo ya biashara bila ruhusa yake.

Katika kesi hiyo ya madai namba 36 ya mwaka 2022, ambayo shahidi wa kwanza ni mwanamuziki huyo, amedai mbele hakimu mwandamizi, Bitony Mwakisu kuwa kampuni hiyo imejinufaisha kwa kutumia wimbo wake wa ‘Tabasamu Tanzania’ kujitangaza kibiashara.

Akiongozwa na wakili wake, Lillian Justo amesema alianza kazi ya sanaa mwaka 2015 na wimbo huo ya Tabasamu Tanzania aliuachia kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari mwaka 2021, na baadaye alikabidhiwa cheti cha umiliki wa wimbo kupitia Chama Cha Hakimiliki (COSOTA).

“Niliona wimbo wangu inatumiwa kutangaza biashara zinazotolewa na kampuni hiyo ya Kilimanjaro, niliurekodi kupitia simu yangu ya mkononi na baadaye nilipeleka malalamiko yangu COSOTA,” amesema mwanamuziki huyo.

Al Hilal kumlipa Neymar mshahara mara sita zaidi ya anaolipwa PSG

Aidha, amesema COSOTA iliandika barua ya wito kwa kampuni ya Kilimanjaro ambapo kampuni hiyo iliwakilishwa na kondakta wake, lakini mazungumzo baina yao hayakufikia mwafaka.

“Niliamua kuiandikia barua kampuni hiyo (Demand Note) ya kusudio la kuishitaki nikitaka inilipe shilingi milioni 123 ndani ya siku 14, hata hivyo hawakujibu chochote na baada ya muda huo niliamua kuja hapa mahakamani kudai haki yangu,” ameeleza.

Send this to a friend