Mshitakiwa wa 3 kesi ya Rugemalira arejeshwa rumande

0
64

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 16, 2021 imemwachia huru Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemarila baada ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali kufuta mashitaka 6 ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yanamkabili tangu mwaka 2017.

Mbali na Rugemalira, wengine waliokuwa kwenye kesi hiyo ambayo jumla ilikuwa na mashitaka 12 ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, Harbinder Seth na mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.

Wakati mfanyabiashara huyo akiachiwa huru leo, Seth aliachiwa huru Juni 16 mwaka huu na kutakiwa kulipa fidia ya TZS 26.9 bilioni baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia TZS 309 bilioni kwa njia ya udanganyifu, na siku ya kuachiwa alianza kwa kulipa TZS 200 milioni.

Wawili hao sasa wakifurahia uhuru wao, hali bado ni ngumu kwa Makandege ambaye anaendelea kusota rumande hadi Desemba mwaka huu baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi yake.

“Kesi naiahirisha hadi Desemba 23, 2021 na mshitakiwa Makandege ataendelea kuwa mahabusu,” amesema Shaidi.

Send this to a friend