Msichana aanza masomo na mwanae wa miezi minne

0
41

Msichana kutoka mkoani Mbeya amelazimia kurudi darasani kuendelea na masomo akiwa na mwanae mchanga kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu lilolotoa ruhusa kwa wote waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kurejea shule.

Esnath Gideon mwenye miaka 19 ameiambia BBC kwamba amekosa mtu wa kumsaidia kukaa na mtoto, na walimu wake wakawa wakarimu kumruhusu kuingia na mtoto wake mwenye miezi minne darasani.

Ameeleza kwamba alipoteza matumaini ya kuhitimu masomo yake alipopata ujauzito akiwa kidato cha nne, lakini sasa anafuraha kufuatia serikali kufungua milango ya waliokatisha masomo kurudi shule na kwamba lengo lake ni kusoma kwa bidii na kuwa Mwanasheria.

“Na mtoto darasani, usikivu wangu unaathiriwa lakini nina uwezo wa kusikiliza. Changamoto ni pale ninapotaka kubadilisha mtoto nepi kwa vile hakuna eneo maalum shuleni kwa ajili ya kumbadilisha,” ameiambia BBC.

Binti huyo anaishi na bibi yake ambaye anauza sambusa sokoni na ameeleza kufurahia sana binti yake kurejea shule.

Bibi ameeleza kwamba alichukizwa sana wakati binti huyo alipopata ujauzito, jambo ambalo lilimaanisha kukatisha masomo.

Ruhusa ya Rais Samia mbali na waliopata ujauzito inawahusu pia walioshindwa kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali au waliofeli.

Send this to a friend