Msichana abakwa, alawitiwa na kuuliwa kwenye mkesha wa mwaka mpya

0
94

Binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Eliza Mlimbila (17) mkazi wa Mtaa wa Sigridi Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe amekutwa ameuawa katika mtaa wa Kahawa baada ya kubakwa, kulawitiwa na kukabwa shingo siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Baba mzazi wa Marehemu, Meshack Mlimbila amedai Jumamosi Desemba 31, 2022 Eliza alichelewa kurudi nyumbani, na alipoulizwa alikuwa wapi aliondoka tena bila kuaga mpaka alipopata taarifa za kifo chake siku ya mwaka mpya.

Dawa za kulainisha choo zinavyochangia mawe kujaa kwenye figo

“Jumamosi tumetoka shambani hatukumkuta nyumbani mpaka saa tatu, aliporudi nikamuuliza lakini alivyotokatoka sikuelewa tena na kwa sababu alikuwa anaweza kutoka na kurudi, mpaka mauti unamkuta sielewi alikuwa wapi.”

Ameongeza, “mara kadhaa tumemuonya lakini sijui ni kwa nini haya magenge yake kwasabu unaweza ukamwambia akakuelewa halafu ukakuta tena hayupo,” amedai baba wa marehemu.

Aidha, Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issah amewahakikishia wananchi kuwa wahusika wote watakamatwa na taratibu zote zitafuatwa ili kushughulikia jambo hilo, huku akiomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi.

Send this to a friend