Msichana wa kazi ashitakiwa kwa tuhuma za kumuua bosi wake

0
39

Msichana wa miaka 15, anayejulikana kwa jina la Sarah Mwendesha amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Mhadhiri wa Kitivo cha Uhandisi cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUTI) mkoani Mwanza, Hamida Mussa.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kumuua mhadhiri huyo maarufu kwa jina la “Mama Mwakitosi” Novemba 29, 2022 kwa kumnyonga kwa kutumia mtandio akiwa nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki.

Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka mtoto wake wa kambo wa miaka mitatu

Inadaiwa kuwa Sarah ambaye alikuwa msaidizi wa kazi za ndani wa mhadhiri huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kukimbilia wilayani Misungwi kabla ya kutiwa mbaroni na maofisa wa polisi siku tatu baadaye.

Mtuhumiwa amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Fortunatus Kubaja kwa ajili ya kusomewa shitaka hilo, hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 19, 2023 itakapotajwa tena.

Send this to a friend