Msigwa: Ahadi ya Rais Samia kununua kila goli TZS milioni 5 inaendelea

0
54

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa pesa kwa kila goli la vilabu vya Simba na Yanga katika mashindano ya kimataifa ni mwendelezo.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio nchini, Msigwa amesema ahadi hiyo ya Rais kiasi cha pesa TZS milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa katika mashindano hayo, itaendelea mpaka mwisho wa mashindano hayo.

Eng. Hersi: Feisal bado hajarudi kambini

Klabu ya Simba na Yanga kwa sasa zinashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Afrika ambapo Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikishiriki katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Februari 19, 2023 Klabu ya Yanga ilipokea pesa taslimu TZS milioni 15 kutoka kwa Rais Samia pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kuunga mkono juhudi za Rais kufuatia magoli 3-1 waliyoyapata dhidi ya TP Mazembe na kukamilisha takribani jumla ya TZS milioni 33.

Send this to a friend