Msigwa: Kipindi cha mpito kwa waandishi kinaisha Desemba 2021
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amewakumbusha wanahabari kuwa kipindi cha mpito kinachowataka wawe na elimu angalau kuanzia ngazi diploma kinaishia Desemba 31, 2021.
Msigwa amesema hilo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) katika ofisi za Idara ya Habari Maelezo zilizopo jijini Dodoma.
Amewatoa hofu wanahabari kuwa wasichukulie hasi kanuni za Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa kuwa ina malengo chanya kwa taaluma ya habari nchini.
“Mtu anayelima muhogo, hawezi kulima tu bila kufuata kanuni bora za ukulima wa muhogo, hivyo itampasa kupata elimu ya namna bora ya kulima ili kupata ama kuongeza tija,” ameeleza Msigwa.
Mwaka 2017 serikali ilitangaza uamuzi huo baada ya kupitia maoni ya wadau mbalimbali waliotoa maoni yao kwa lengo la kuboresha tasnia ya habari.