Msigwa: Rais Samia amechangia pakubwa kukamilika kwa Ikulu Chamwino

0
55

Serikali imesema inajivunia mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino jijini Dodoma ambao utaandika historia nyingine nchini Tanzania.

Akizungumza Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia ameonesha ushujaa katika kukamilika kwa ujenzi wa ofisi za Rais ambao unatarajiwa kuzinduliwa Mei 20, mwaka huu.

“Ofisi ya Ikulu Dodoma imekamilika, ofisi hii ndiyo ambayo Rais Dkt. Samia ataitumia kwa kazi zake za kila siku. Tunafahamu Ikulu ya Dar es Salaam ilijengwa wakati wa ukoloni, hivyo hatua ya ujenzi huu kujengwa kwa fedha za ndani kwa kutumia vijana wetu wa JKT na kukamillika hadi kufikia kuzinduliwa mapema mwezi huu.

Rais Samia ameimarisha kwa kasi huduma ya maji mijini na vijijini

Serikali tutaendelea kutambua mchango wa Rais Samia kama shujaa katika kuandika historia hii muhimu,” amesema.

Aidha, ujenzi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa mji wa Serikali jijini Dodoma ambao umefikia asilimia 60 hadi 70, ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 1973 kuhusu Serikali kuhamia mkoani humo.

Msigwa ameeleza kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa mji wa Serikali ulihusisha majengo 24 ya chini, na awamu ya pili iliyozinduliwa hivi karibuni itahusisha ujenzi wa majengo 28 ya maghorofa, ofisi za wizara na wafanyakazi wote wa ofisi za Serikali.

Send this to a friend