Msigwa: Tanzania haina wafungwa wa kisiasa

0
56

Serikali imewataka Watanzania kupuuza taarifa zinazosambazwa na chombo cha habari kutoka Kenya kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuachiwa huru kwa wafungwa 23 wanaodaiwa kuwa ni wa kisiasa.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam na kusisitiza kuwa Tanzania haina wafungwa wa kisasa.

“Kuna clip inazunguka ikisema Rais Samia Suluhu ametoa agizo la kuachiwa huru kwa wafungwa wa kisiasa 23, sio kweli Rais hajazungumza suala hilo. Pili, nchi yetu haina Wafungwa wa Kisiasa,” amesema Msigwa

Aidha, amesema anaamini chombo hicho ambacho hakukitaja, kitaomba radhi na kufuta taarifa hiyo. ” Tayari ofisi yetu ya ubalozi Nairobi inafuatilia kujua kwanini wamepotosha.”

Katika hatua nyingine amewasihi waandishi wa habari kufuata kanuni za uandishi wanapoandika habari zote, na sio kukimbilia kuchapisha bila kupata ufafanuzi.

Send this to a friend