Msisikilize maneno ya watu wa pembeni, Waziri Mkuu awaambia wakazi wa Ngorongoro

1
41

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea mapendekezo kutoka kwa wananchi wa tarafa za Loliondo, Ngorongoro na Sale kuhusu namna bora ya kulinda uhifadhi wa maeneo hayo.

Maoni hayo yaliwasilishwa kwa Waziri Mkuu na wawakilishi wa wakazi wa wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Shangai, Madiwani, wenyeviti wa vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana ofisini kwake Mlimwa, Dodoma.

Akizungumzia kuhusu eneo la Msomera lililoko wilayani Handeni, Tanga ambako yanaandaliwa makazi kwa ajili ya kuwahamishia wakazi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiari amesema ujenzi unandelea vizuri.

Baada ya kupokea mapendezo hayo, Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao kwani haiwezi kuwa na mipango mibovu kwa wananchi wake na kuwasisitiza, “Msisikilize maneno maneno ya watu wa pembeni.”

Hata hivyo ameongeza kuwa ujenzi wa nyumba za makazi 103 upo mbioni kukamilika na Serikali imepanga kuongeza nyumba nyingine, lengo likiwa ni kufikia nyumba 500 kwa ajili ya wakazi hao.

Kadhalika, Majaliwa amesema Serikali inaendelea kuimarisha sekta ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wote nchini wanapata tija kupitia shughuli hiyo.

Send this to a friend