Msumbiji yahusishwa kwenye mlipuko uliotokea mjini Beirut

0
48

Serikali ya Msumbiji imesema haikuwa inafahamu chochote kuhusu meli iliyokuwa imebeba mzigo wa ammonium nitrate inayodaiwa kusababisha mlipuko mjini Beirut, Lebanon na kusababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali.

Taarifa zinadai kuwa meli hiyo iliyong’oa nanga katika Bandari ya Beira, nchini Msumbiji ilishusha mzigo mjini Beirut mwaka 2013 uliohifadhiwa katika ghala ya bandari.

“Mamlaka ya bandari haikuwa inajua kuwa Meli ya MV Rhosus ilibakisha mzigo baada ya kutoka Bandari ya Beira,” imeeleza mamlaka ya bandari ya Beira.

Mamlaka hiyo imesema utaratibu ni kuwa kunapaswa kuwepo kwa taarifa ya kuwasili kwa meli kati ya siku saba hadi 15 kabla ya kuwasili, lakini hakukuwa na taarifa za meli hiyo.

Maafisa wa bandari wameongeza kuwa safari ya meli hiyo haikupaswa kuishia Msumbiji bali Zimbabwe au Zambia, kwa sababu ilikuwa imebeba kemikali inayotumika kutengeneza mlipuko kwa ajili ya sekta ya migodi.

Send this to a friend