Msuva: Sina mpango wa kucheza ligi ya Tanzania

0
69

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ameweka wazi matamanio yake ya kuendelea kucheza nje ya nchi baada ya tetesi ya kuhusishwa kujiunga na klabu za Yanga, Simba na Azam.

Msuva amesema timu zote zimewahi kumuomba ajiunge nazo lakini aliwaweka wazi kuwa lengo lake ni kucheza nje ya Tanzania.

Geita yamalizana na FIFA

Mchezaji huyo amesema mpaka sasa ana asilimia nyingi za kucheza nje ya nchi na mara atakapokuwa tayari ataweka wazi ni timu gani atakwenda kujiunga nayo.

Msuva amewahi kuchezea Yanga michezo 94 ambayo alifanikiwa kufunga magoli 43 kabla ya kuhamia timu ya Difaa El Jadida na baadaye Wydad Casablanca, zote za Morocco.

Send this to a friend