Mtaalam: Ukiathiriwa na sumu usinywe maziwa, njoo hospitali au tupigie simu

0
26

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeitaka jamii kwenda hospitali au kuwasiliana na Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu pale wanapokumbwa na matukio hayo badala ya kukimbilia kunywa maziwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkuu wa kituo hicho, Yohana Goshashy amesema mtu akikumbwa na tukio kama hilo asikimbilie kunywa maziwa kwa sababu baadhi ya sumu zikikutana na majimaji madhara yanakuwa makubwa.

Serikali yaondoa ‘expire date’ kwenye vitambulisho vya Taifa

“Mtu anaweza kunywa sumu kwa bahati mbaya au akanyeshwa, baadhi ya watu hukimbilia kutapishwa, kunyweshwa maziwa tukifiri hicho ni kiua sumu, hilo halistahili, inabidi kwanza kupata uelewa kutoka kituo cha kudhibiti matukio ya sumu ama hospitali ya karibu,” amesema.

Goshashy anaeleza kuwa kuna baadhi ya sumu hupunguzwa ukali kwa kunywa maji hivyo mtu anapotumia maziwa kama njia ya kuipunguza inaweza isimsaidie.

Send this to a friend