Msimamizi wa upimaji virusi vya Corona Kenya ashushwa cheo

0
35

Kushushwa cheo kwa mtaalamu aliyekuwa anahusika na upimaji wa sampuli za virusi vya corona nchini Kenya kumeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wenzake.

Dkt. Joel Lutomiah alikuwa Mkurugenzi wa taasisisi ya uchunguzi wa virusi, ambapo wizara ya afya imesema kuwa wameshushwa cheo kutokana na kucheleshwa kwa majibu ya sampuli pamoja na masuala mengine ya kiuongozi.

Wakati serikali ikisema hayo, wanasayansi wamesema kuwa Dkt Lutomiah ameondolewa madarakani kutokana na msimamo wake wa kuitaka serikali kuiwezesha kifedha Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya pamoja na kuipatia vifaa muhimu.

Watafiti wenzake wamesema kuwa Dkt Lutomiah alitishia kusitisha upimaji wa sampuli za corona endapo serikali isingewapatia vifaa tiba.

Hadi Aprili 27, 2020 asubuhi, Kenya ilikuwa na visa 355 ambapo kati ya hivyo, watu 106 wamepona na 14 wamefariki dunia.

Send this to a friend