Mtaalamu: Wanawake wanachangia ongezeko la tatizo la nguvu za kiume

0
53

Kutokana na idadi ya wanaume wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume kuongezeka nchini kutokana na sababu mbalimbali zinazotajwa na wataalam wa afya ikiwemo magonjwa, msongo wa mawazo, ulaji na mengineyo, hali ambayo inazidi kuleta athari kubwa kijamii na kihisia.

Akizungumza na Swahili Times, Mwanasaikolijia kutoka Care Health Tanzania, John Ambroce anasema kuwa wanawake ni moja ya chanzo cha kukua kwa tatizo hilo kwa baadhi ya wanaume wanaosumbuliwa na tatizo hilo.

“Mwanamke anachangia tatizo kwa namna ambavyo analeta udhalilishaji, ukosoaji, kufedhehesha na kumuumiza kutokana na hilo jambo ambalo linatokea,” ameeleza.

Mwanasaikolojia anasema wanaume wenye changamoto hiyo ambao wamepata ushirikiano kutoka kwa wake zao, wamepata ufumbuzi wa haraka ukilinganisha na wanaume ambao hawakupewa ushirikiano.

“Kwa wale ambao wameweza kushirikiana na wanaume, jinsi anavyolipokea hali hiyo, ile ndio tiba kubwa kushinda matibabu mengine unayoweza kuyafikiria. Lakini pia muda mwingine tunapozungumzia kwamba kuna tatizo inawezekana halipo bali ni ile hofu ambayo tunakuwa nayo,” anaeleza.

JWTZ yamsaka aliyesambaza uzushi mitandaoni

Aidha, amesema wanaume wengi wanapata msongo wa mawazo unaosababishwa na wake zao nyumbani lakini pia wengine wanakosa haki zao za ndoa na kupelekea kutumia njia isiyo sahihi ambayo inaua nguvu za kiume.

“Mwingine anapata mwanamke ambaye yuko bize sana na mwingine anampa mwenza wake ratiba kwamba mimi mpaka wikiendi, sasa hapa katikati kama yeye si mtu wa kuchepuka anafanya ‘masturbation’ [punyeto] na hiyo si nzuri,” ameeleza.

Send this to a friend