Mtambo wa kwanza JNHPP waanza kuzalisha umeme

0
33

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo ameshuhudia kuwashwa kwa mtambo wa kwanza katika Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na kuingiza megawati 235 kwenye Gridi ya Taifa.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo amesema kuingia kwa megawati 235 kunafanya mgao wa umeme kupungua kwa asilimia 85 nchini.

“Ninafurahi kusema kile ambacho tuliahidi kufikia Februari 25 tutakuwa tumeingiza umeme wa mtambo namba tisa, kimekamilika,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa mtambo namba nane unatarajiwa kukamilika Machi na kufanya jumla megawati 470 kuingia kwenye gridi ya Taifa.

Ameongeza kuwa kazi ilipaswa kukamilika mwezi wa sita lakini kutokana na msukumo uliowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan umefanya kazi kukamilika kabla ya wakati.

“Tunamshukuru sana Rais kwani wakati anaingia madarakani mradi huu ulikuwa asilimia 33, amefanya kazi kubwa kuhakikisha fedha za mradi zinapatikana kwa wakati,” amesema Dkt. Biteko.

TagsMtambo
Send this to a friend