Mtangazaji B-Dozen wa Clouds FM atimkia E-FM

0
72

Mtangazaji maarufu wa Clouds FM (Clouds Media Group), Hamisi Mandi amejiunga rasmi na kituo cha utangazaji cha E-FM (E-FM Company Limited).

Mandi ambaye anafahamika zaidi kwa jina la utangazaji la B-Dozen (The Navigator, Msafiri) kwa muda mrefu alikuwa akiongoza kipindi cha XXL cha Clouds FM, pamoja na vingine.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, E-FM wameandika mbobezi huyo wa utangazaji amejiunga nao, na kwamba kinachofuata ni kupaa juu, na kuhakikisha mafanikio zaidi kwa Tanzania.

Vituo hivyo viwili vya redio kwa miaka kadhaa sasa vimekuwa na ushindani wa kibiashara katika muziki, ambapo watangazaji wamekuwa wakihama na kuhamia kutoka vituo hivyo.

Mwanzoni mwaka 2016 watangazaji watatu wa Clouds FM, Gerald Hando, Paul James (PJ) na Abel Onesmo walihama na kujiunga E-FM, lakini mwishoni mwa mwaka huo, PJ alirejea Clouds FM akitokea E-FM.

Send this to a friend