Mtangazaji Gerald Hando aadhibiwa na EFM

0
14

Mtangazaji Gerald Hando aadhibiwa na EFM

 

Uongozi wa EFM na TVE imechukua hatua dhidi ya Mtangazaji Gerald Hando kufuatia kauli yake aliyetoa katika kipindi cha Joto la Asubuhi.

Kauli yake ilinukuliwa Desemba 27, 2022 akisema kuwa hapendi Serikali inavyokopakopa na kwamba maisha magumu wanayopitia wananchi yanasababishwa na Serikali kukopa.

“Kwa kutambua upungufu huo, EFM na TVE imechukua hatua dhidi ya mhusika na tunapenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wote waliokwazika na kauli hiyo,” imesema taarifa hiyo.

Mmiliki wa kituo hicho, Francis Majizzo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema “mimi kama mfanyabiashara, naelewa zaidi suala la mikopo. Biashara zangu katika udogo wake, zinaendelea kukopa na kudaiwa; sembuse nchi yenye watu milioni 61?”

Licha ya maelezo yake kuwa anaheshimu mtazamo wa Hando, lakini haiubaliani nao kwani “Namna na mahali ulipowasilishwa pia unaibua maswali ya kitaaluma, na kutoka na hayo tunaomba radhi, na kuahidi kupata majibu kitaaluma.”

Send this to a friend