Mtangazaji wa Clouds TV ateuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida

0
17

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya (6) kama ifuatavyo;

Kwanza, amemteua Bw. Hassan Nassoro Ngoma kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida Mkoani Singida. Anachukua nafasi ya Bw. Wilson Samwel Shimo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita.

Pili, amemteua Bw. Kamana Juma Simba kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, Mkoani Arusha. Anachukua nafasi ya Bw. Toba Alnason Nguvila ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Tatu, amemteua Bi. Faraja Pascal Msigwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha. Anachukua nafasi ya Bw. Abbas Kayanda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu.

Nne, amemteua Bw. Bahati Joram kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro. Anachukua nafasi ya Bw. Lameck Michael Lusesa.

Tano, amemteua Salum Halfan Mtelela kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara. Anachukua nafasi ya Bw. Jonas Nyehoja aliyestaafu.

Sita, amemteua Bw. Augustino Chazua kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro. Anachukua nafasi ya Bw. Robert Francis Selasela.

Wote wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dodoma siku ya Jumatano tarehe 8/7/2020 saa 4:00 asubuhi.

Send this to a friend