Mtanzania afariki kwa Ebola nchini Uganda

0
37

Daktari ambaye ni raia wa Tanzania (37) aliyekuwa akisomea Shahada ya Uzamili ya Udaktari kwenye Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa Afya nchini humo, Dkt. Jane Ruth Aceng amesema Dkt. Mohammed Ali aligundulika kuwa na Ebola Septemba 26, 2022 na alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Fort Portal.

Taarifa zinasema haijabainika jinsi alivyoambukizwa, lakini kifo chake kinajiri saa chache baada ya Wizara ya Afya kutangaza kuongezeka kwa idadi ya waliofariki kutokana na mlipuko huo hadi kufikia saba.

“Ni kwa masikitiko makubwa tumepokea taarifa za kufariki kwa Dkt. Mohammed Ali, raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 37 ambaye alikuwa akisomea Shahada ya Uzamili ya Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala. Dkt. Ali alishindwa katika vita dhidi ya ugonjwa wa Virusi vya Ebola,” kimeandika Chama cha madaktari kwenye ukurasa wao wa Twitter.

Chanzo: BBC Swahili

Send this to a friend