Mtanzania aja na teknolojia ya kutengeneza barabara za lami kwa udongo

0
53

Joseph Katallah, Mtanzania anayeishi nchini Canada kwa kushirikiana na kampuni ya Geopolymer Solutions LLC ya nchini Marekani ameonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania kwenye ujenzi wa barabara za lami kwa kutumia teknolojia mpya iliyogunduliwa na kampuni hiyo.

Wawekezaji hao ambao wako nchini kwa ajili ya ziara ya wiki mbili, wameeleza kuwa Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kupewa kipaumbele katika uwekezaji wa teknolojia hiyo ambayo itahusisha matumizi ya udongo mwekundu balada ya kutumia saruji ya kiwandani.

Katika kikao kilichokutanisha wawekezaji pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wawekezaji wameeleza umuhimu wa teknolojia hiyo kufanyiwa majaribio katika maeneo korofi na kueleza ufanisi wa teknolojia hiyo katika maeneo mengi korofi ambayo kampuni zenye teknolojia nyingine zimeshindwa kukidhi na kudhibiti changamoto hiyo.

Hata hivyo wataalamu kutoka sekta ya barabara wameeleza kuwa ni vema uwekezaji wa aina hiyo ukafuata taratibu zilizowekwa na mfumo wa Serikali, na kuruhusu kufanyika kwa tafiti inayopimika ili kujiridhisha na ufanisi wake katika ardhi na hali ya hewa ya Tanzania.

Send this to a friend