Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya China

0
13

Raia wa Tanzania aliyefahamika kwa jina moja la Dossa amekamatwa katika Mji wa Macau, China kwa madai ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine.

Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa raia huyo aliyekua akiendelea kukaa nchini humo licha ya muda wake kuisha amekamatwa akiwa na gramu 15 za cocaine, takribani gramu 2.5 za dawa ambazo hazijulikani na fedha takribani TZS 9.6 milioni zilikutwa kwenye makazi yake.

Dawa zilizokamatwa zimeripotiwa kuwa na thamani ya TZS 14.4 milioni.

Afisa wa serikali nchini humo,Lei Hon Nei amesema Dossa mwenye umri wa miaka 39 ana hati ya kusafiria ya Tanzania na alikaa nchini humo licha ya kibali chake kumalizika.

Lei amesema maafisa wa forodha wa wa Hong Kong walitoa taarifa kuhusu kipeto chenye uzito wa 1kg kilichowasili Macau kutoka Ulaya. Kwa mujibu wa Idara hiyo, kipeto hicho kilikuwa na cocaine na Dossa ndiye mpokeaji na alieleza alipo.

Mtuhumiwa huyo amesema kuwa alinunua dawa hizo kutoka mgeni mjini Macau kwa 290,000 kwa ajili ya matumizi binafsi. Mtuhumiwa allikanusha kusafirisha dawa hizo na alipopimwa akakutwa na cocaine mwilini.

Anashtakiwa kwa matumizi haramu na usafirishaji wa dawa za kulevya.

Send this to a friend