Mtanzania aliyetekwa Nigeria aachiwa huru

0
53

Frateri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma, Merikiori Mahinini (27) aliyekuwa ametekwa nyara na watu wasiojulikana nchini Nigeria ambako alipelekwa na Shirika la Wamisionari wa Afrika kwa ajili ya mwaka wa uchungaji ameachiwa huru.

Mtanzania huyo aliyetekwa na kikundi cha watu wasiojulikana akiwa pamoja na mwenzake raia wa Mali wameachiwa huru usiku wa kuamkia Agosti 24 wakiwa salama.

Akizungumzia kuachiwa huru kwa Mtanzania huyo, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Dkt. Benson Bana amesema njia zote zilitumika kuhakikisha kwamba kijana huyo na mwenzake wanapatikana wakiwa hai na wamefanikiwa kuwaokoa vijana hao wakiwa salama na sasa wanafanyiwa uchunguzi wa afya zao.

JWTZ yatoa siku saba wenye sare za jeshi au nguo zinazofanania kuzisalimisha

“Wote wako salama, wamedhoofika tu lakini ni wazima. Merikiori anachechemea kidogo kwa sababu wakati wanawaokoa aliruka dirishani akaumia mguu kidogo, lakini yuko salama,” amesema Balozi Bana.

Frateri huyo alikamatwa Agosti 4 mwaka huu katika jimbo la Minna huko Nigeria akiwa na mwenzake Padri Paul Sanogo ambapo watekaji waliamuru wapewe Naira milioni 100 (sawa na TZS milioni 325.1) ili kuwaachia huru wote wawili.

Send this to a friend