Mtanzania aondolewa mbio za mita 100 Uingereza

0
56

Mwanariadha Mtanzania katika mashindano ya mbio fupi kwa wanawake, Winfrida Makenji ameondolewa kwenye mashindano baada ya kukutwa na kosa katika kuanza mbio za mita 100 katika uwanja wa michezo wa Alexander jijini Birmingham, Uingereza.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 21, ameelezwa na kocha wake, Suleiman Nyambui kwamba ni mkimbiaji hodari ila hofu ya mashindano pamoja na kukosa uzoefu wa kushindana mara kwa mara vimechangia kuondolewa kwake mwanzoni tu mwa mbio hizo.

Diamond aeleza sababu ya kuchukua 60% ya mapato ya wasanii WCB

Nyambui amesema Winfrida alifanya kosa la kuchomoka kabla ya mlio wa bastola ya kuanzia kulia, ambapo katika mashindano makubwa kama hayo adhabu yake ni kutolewa (disqualified).

Winfrida amebakiza mchuano wa mbio za mita 200 ambao atashindana Agosti 4, 2022, ambapo atakimbia raundi ya kwanza na kama atafanikiwa kupita ataingia raundi ya pili siku ya pili Agosti 5.

Send this to a friend