Mtanzania ateuliwa kuongoza mamlaka ya mapato Sudan Kusini
Raia wa Tanzania, Dkt. Patrick Mugoya ameteuliwa kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Sudan Kusini (NRA).
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 6 mwaka huu mjini Juba baada ya kusaini mkataba, Dkt. Mugoya amesema atatengeneza mpango mkakati wa kuwezesha uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato yasiyotokana na mafuta.
Amesema majukumu yake ya kwanza ni kuhakikia NRA inafanya kazi kwa ufanisi, kujenga ushirikiano na wadau mbalimbali katika ukusanyaji wa mapato kwa uwazi, uwajibikaji na uhakika pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato kama vile ukwepaji kodi, misamaha ya kodi isiyo na tiha na ingizaji bidhaa kinyemela.
Dkt. Mugoya amewahi kuwa Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).