Mtoto (14) asimulia alivyobakwa na baba yake mzazi

0
98

Mahakama ya Wilaya ya Chunya koani Mbeya imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, Ayub Jackson (34), mkazi wa Kijiji cha Mlima Njiwa baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.

Akitoa ushahidi mahakamani hapo, mtoto huyo (jina limehifadhiwa) aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio baba yake alimvuta chumbani kwake kisha kumvua nguo za ndani na kumwingilia kimwili hivyo kumsababiashia maumivu na kutokwa damu nyingi sehemu zake za siri.

Dawa ya ‘mkongo’ yapigwa marufuku

Anadai, baada ya mama yake kuwasili alimweleza kitendo alichofanyiwa na baba yake, kisha walikwenda kutoa taarifa katika ofisi ya Kijiji na kupelekwa kituo cha Polisi Chunya ambapo alifanyiwa uchunguzi ambao ulibainisha kuwa amefanyiwa kitendo hicho.

Baada ya ushahidi huo, mshtakiwa alikana madai hayo na kujitetea kuwa siku ya tukio alikuwa safarini Mbeya, na kuwasilisha tiketi za basi ambazo zilitumika kama kielelezo.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi, James Mhanusi alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka hivyo mshatakiwa kupatikana na hatia.

Send this to a friend