
Mtoto Sofia Ndoni (3) amefariki dunia kwa madai ya kushambuliwa kwa kipigo kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake kwa fimbo na mpira wa bomba kisha kukabwa shingo na bibi yake aitwaye Christina Kishiwa.
Mtoto huyo alikuwa akiishi na bibi huyo ambaye ni mama mdogo wa mama yake mzazi katika Mtaa wa Nyakato, Kata ya Nyasubi, Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Janeth Magomi, amesema kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha mauaji hayo kinatokana na hasira za mtuhumiwa baada ya mtoto huyo kutomsalimia asubuhi na jioni pamoja na kujikojolea.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea na msako wa kumpata mtuhumiwa huyo ambaye alitoroka baada ya kufanya mauaji hayo.






