Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Consolata Charles, mkazi wa Kijiji cha Mkuyuni, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi amefariki dunia nyumbani kwa mchungaji alipokuwa akifanyiwa maombi.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Azam TV Consolata aligundulika na ugonjwa wa malaria pamoja na typhoid ambapo alipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Katavi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Inadaiwa kuwa baada ya kupatiwa matibabu alipewa ruhusa ya kurejea nyumbani, na baada ya siku chache afya yake ilizidi kudhoofika ndipo wazazi wake waliamua kumpeleka katika nyumba ya mchungaji ili aweze kupata huduma ya maombi.
Anayejiita ‘Yesu’ Kenya akimbilia polisi, wananchi wataka kumsulubisha Pasaka
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkuyuni, Gitan Chembanenge amethibitisha kuwa ni kweli marehemu alikuwa mgonjwa, na baada ya kupelekwa kufanyiwa maombi ndipo mauti yalipomkuta.