Mtoto aliyesaidiwa matibabu ya ngozi na Rais Samia atoka hospitali

0
89

Mtoto Aminu Baranyikwa (15) aliyesaidiwa matibabu ya ngozi na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akiwa ziarani mkoani Kagera ameruhusiwa kutoka hospitalini na kwenda nyumbani.

Mtoto huyo aliyekuwa ameketi kando ya barabara Oktoba 2022 wakati wa msafara wa Rais Samia ukipita eneo hilo huku  ngozi yake ikiwa imeharibika vibaya kwa maradhi, Rais Samia aliwaagiza wasaidizi wake wamfuate na kumdadisi kwa kina.

Baada ya kumdadisi mtoto huyo, Rais Samia aliagiza apelekwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Aminu amemshukuru Rais Samia kwa msaada wake aliompatia huku akiomba apewe msaada wa masomo kwani familia yake ni ya hali ya chini na haiwezi kumudu gharama za masomo yake.

Send this to a friend