Mtoto anywa sumu baada ya kufokewa na baba yake kisa Punda

0
49

Mtoto mmoja amekutwa amefariki kwa kunywa sumu wilayani Makete, mkoa wa Njombe baada ya kufokewa na baba yake aliyekuwa akimuonya baada ya kuwaacha punda waliokwenda kula mazao kwenye shamba la watu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema mtoto huyo aliacha punda aliokuwa nao machungani na kwenda kucheza na watoto wenzake, hali iliyomfanya baba yake kumuonya baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mwenye shamba.

“Huyu Mtoto alipewa punda akachunge, akawaacha na akaenda kucheza, na matokeo yake wale punda wakala shamba la mtu, mzee wake akalalamikiwa ndipo akamwita mtoto, lakini kitendo cha mzee kumfokea yule mtoto achunge punda kwa umakini, yeye akachukua maamuzi magumu akatafuta sumu akanywa na kufariki,” ameeleza Issah.

Aidha, ametoa wito kwa wazazi na walezi kutafuta njia sahihi ya kuzungumza na watoto wao, huku akiomba makanisa na misikiti kuendelea kutoa mafunzo mema ya dini kwa watoto ili kuepuka kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Send this to a friend