Mtoto ashikiliwa kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake Njombe

0
62

Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Mahamoud Banga amesema Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia mtoto wa miaka 12 kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa darasa la nne (10) katika shule moja iliyopo Makambako mkoani Njombe.

Kamanda Banga amebainisha kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akilawitiwa kwa ahadi ya kupewa fedha na mtuhumiwa huyo ambaye aliacha shule akiwa darasa la sita.

“Mtuhumiwa huyu anaonekana aliacha shule akiwa darasa la sita lakini amekuwa akimfanyia hivi vitendo kwa muda mrefu kwa ahadi ya kumpatia fedha,” amesema Kamanda Banga wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Aidha, ameeleza kuwa kwa muda wote huo mwanafunzi huyo aliyefanyiwa ukatili huo hakuwaeleza wazazi wazazi wake, lakini tabia yake ilianza kubadilika baada ya kuwa anatokwa na haja kubwa, na baada ya mama yake kumuadhibu, ndipo alisema kuwa anafanyiwa vitendo hivyo.

Send this to a friend