Mtoto atolewa sarafu iliyokwama kooni

0
13

Wataalamu katika Idara ya ENT ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) wamefanikiwa kuitoa sarafu iliyokuwa imekwama kwenye koo la mtoto mdogo kwa siku sita.

Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo wa BMH, Emmerenceana Mahulu, amesema BMH imempokea mtoto huyo wa miaka miwili siku ya Alhamisi ya tarehe 26, Machi.

Dkt. Mahulu amefafanua kuwa sehemu ya koo ilipokuwa imekwama sarafu ilisababisha uvimbe, akiongeza kuwa ilikuwa imeacha uwazi kidogo ambayo ilikuwa ikiruhusu vimiminika kama uji, maji juisi kupita.

Kwa mujibu wa mama wa mtoto, Juliana Yuda, mkazi wa kijiji cha Mkoka, Kongwa, Dodoma, mtoto wake, ambaye alitoka kucheza na wenzake siku ya Jumamosi ya tarehe 20, Machi, alirudi nyumbani muda wa mchana akiwa analia.

“Mtoto alikuwa hawezi kula kwa muda wa siku sita, alikuwa anashindia uji, juisi na maji tu. Hali yake ilizidi kuwa mbaya Siku ya Alhamisi,” anasema.

Anaongeza kuwa Alhamisi ya tarehe 26, Machi alimpeleka mtoto Hospitali ya Wilaya ya Kongwa ambapo alipewa rufaa kuja BMH baada ya kupigwa picha ya x-ray na kubaini sarafu imekwama kwenye koo. Mtoto huyo sasa ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya matibabu.

Send this to a friend