Mtuhumiwa wa mauaji Kenya ashinda ubunge

0
40

Mwanasiasa anayetuhumiwa kwa mauaji nchini Kenya, Didmus Wekesa Barasa ametetea kiti chake cha ubunge kwa tiketi ya chama cha United Demokratic Alliance.

Barasa ambaye anatuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake, Brian Khaemba wa chama cha DAP-K Jumanne jioni, amepata kura 26,000 dhidi ya kura 9000 za Khaemba.

Inadaiwa, mbunge huyo ametorekea nchini Uganda ili kukwepa mkono wa sheria huku polisi nchini humo wakiwa macho kumkamata endapo angefika katika kituo cha kuhesabia kura.

Baadhi ya wananchi nchini humo wamemtetea mbunge huyo dhidi ya madai hayo, wakisema mbunge huyo alikuwa anajilinda.

“Bw. Barasa alikuwa anajilinda, hii si mara ya kwanza kwa watu kujaribu kumuua,” mmoja wa wananchi Kenya.

Hapo awali, maafisa wa polisi walimkamata afisa msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Lwanda katika jimbo la Kimilili kwa madai ya kuvuruga kura za urais.

Hata hivyo, aliachiliwa baada ya maafisa wa IEBC na polisi kugundua kuwa kituo hicho kilikuwa na maeneo mawili ya kupigia kura.

Send this to a friend