Mtuhumiwa wa wizi afariki mikononi mwa Polisi

0
39

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kifo cha mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kibabu Msese (26) mkazi wa Karatu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo amesema Mei 11 mwaka huu marehemu alikamatwa na watu wengine wanne kwa tuhuma ya unyang’anyi wa kutumia silaha lililotokea Kibaoni, Karatu.

Amesema mfanyabiashara wa M-Pesa na mkazi wa Manyara Kibao Innocent Olotu alivamiwa na kundi la majambazi hao na kuporwa fedha kiasi cha TZS milioni 14.59, simu kadhaa pamoja mashine za uwakala wa benki.

Ufuatiliaji ulifanyika na kuwakamata watuhumiwa mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Arusha, na wakati wa mahojiano watuhumiwa hao walionesha baadhi ya mali zillizoibiwa pamoja na silaha waliyokuwa wanaitumia katika tukio hilo, pia walikiri kushiriki matukio kadhaa nje na ndani ya Mkoa na walifikishwa mahakamani Mei 27, 2022 ambapo watuhumiwa wengine wanaendelea kutafutwa.

Aidha, hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali ya Karatu Mei 5, 2022 na kisha Mei 25 mwaka huu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kwa matibabu zaidi, na kufariki Mei 31 2 wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Jeshi la polisi limesema uchunguzi umeanza kwa kushirikisha vyombo vingine kubaini chanzo cha kifo hicho, na kutoa wito kwa ndugu wa marehemu kuwa watulivu wakati Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Send this to a friend