Mufti awashauri Watanzania kuacha dhambi ili mvua zinyeshe

0
48

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaasa Watanzania kupunguza na kuacha kabisa kutenda dhambi na badala yake wamrudie Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na adha ya ukame ulioikumba nchi.

Ameyasema hayo leo Novemba 5, 2022 alipokuwa akiongoza dua maalum ya maadhimisho ya miaka 26 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

Mwalimu wa Madrasa adaiwa kulawiti watoto 10 aliokuwa anawafundisha

Mufti Zubeir amesema kukosekana kwa mvua, uwepo wa ukame na kukauka kwa maji ardhini ni ishara kwamba watu wanatenda maasi.

“Tunapoomba mvua tuendelee kuacha maasi na mambo mengine yasiyofaa, watu waache dhuluma, mambo mabaya yanayosababisha sisi Mwenyezi Mungu atunyime mvua,” amesema Mufti Zubeir.

Send this to a friend