Mufti wa Tanzania: Msichague viongozi kwa mrengo wa dini

0
41

Siku tano kabla ya Watanzania kufanya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuchagua viongozi kwa kuangalia sera na si kwa mrengo wa dini.

Hayo yamesemwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hamis Mtupa ambaye alikuwa mwakilishi wa Sheikh Zuber na kuongeza kuwa licha ya kuwa Watanzania wana dini, Tanzania haina dini.

Aidha, amewataka Watanzania wote bila kujali dini zao kuhakikisha wanazingatia uwepo wa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Send this to a friend